23 Oktoba 2025 - 17:15

Jamiatul Mustafa (s) Tanzania |  Darasa la Qur’ani Tukufu – Alhamisi, 23 Oktoba 2025 - Mwalimu: Sheikh Muhammad Ja‘fari

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Darasa la kila wiki la Qur’ani Tukufu limefanyika kama ilivyo kawaida chini ya uongozi wa Mwalimu Sheikh Muhammad Ja‘fari.
Lengo kuu la darasa hili ni kukuza uelewa sahihi wa Qur’ani, kuboresha ustadi wa kusoma na kutamka kwa usahihi, pamoja na kuwahamasisha vijana na waumini kwa jumla kujifunza kwa mapenzi elimu na mafunzo yaliyomo katika Kitabu kitukufu cha Allah (s.w.t).

Wanafunzi walishiriki kwa ari na nidhamu, ambapo mwalimu alisisitiza umuhimu wa kutafakari maana za aya na kuzihusisha na maisha ya kila siku.
Darasa liliendelea kwa mazoezi ya tajwidi, tafsiri ya baadhi ya aya, na maswali ya kujadili kuhusu mafunzo ya kiroho na kimaadili yanayopatikana katika Qur’ani.

Kwa jumla, kipindi kilimalizika kwa dua fupi ya kuomba tawfiq na istiqama katika njia ya elimu na uongofu wa Qur’ani Tukufu.

Jamiatul Mustafa (s) Tanzania |  Darasa la Qur’ani Tukufu – Alhamisi, 23 Oktoba 2025 - Mwalimu: Sheikh Muhammad Ja‘fari

Your Comment

You are replying to: .
captcha